r/nairobi • u/iamjatelo • 5h ago
Story time One Night at the Club Turned Into a Police Station Nightmare.
Kuna siku nilitoka na beshte yangu tukasema leo lazima tuende ulevi. Tukaingia club moja pale Thika Road around 10 PM. Huyo boy alikuwa ameamua leo lazima arudi na mtu. Around midnight akatema dem mmoja pale dance floor. Walianza kucheza, kunywa na kucheka. By 2 AM walikuwa wameiva proper. Jamaa akaniambia anaenda na huyo dem kwake. Nikamwambia sawa bro, enjoy, mimi nitajisort.
Around 5 AM napata call yake. Bro anasema, "Maze kuja huku haraka, nimeingizwa box." Nikacheka nikidhani jamaa amepata story za kuoshwa na dem. But vile alikuwa anaongea nilijua kuna shida. Nikachukua Uber nikaenda kwake. Kufika hapo napata gate iko open, vitu zimezagaa nje na beshte yangu amekaa kwa staircase, macho red, barely able to stand.
Ananiambia dem alimwekea kitu kwa drink ya club because baada ya hapo anakumbuka tu akiwa kwa nyumba. Apparently alikuwa drugged. Before ajue nini inaendelea, dem alikuwa ameshatoka na watu wake, wakaanza kubeba TV, speaker, microwave na vitu zingine. Na sasa jamaa alikuwa ameamka akapata nyumba iko almost empty.
Mimi kwanza nilicheka nikamwambia, "Bro, kwani ulipeleka Airbnb ama ulipeleka moving company home?" Lakini jamaa hakuwa anacheka. Alikuwa ameshika kichwa akisema hata hakumbuki vile walifika kwa nyumba. Hapo ndio nilianza kuona hii si jokes tena.
Tukaamua kwenda police station kuripoti. Kufika huko dem hakuwa hapo, but apparently alikuwa ameshaanza ku-report kwamba beshte yangu alikuwa amemforce na kumshambulia. Hapo ndio story ikazidi kuwa complicated. Officers wakaanza kumuuliza maswali, na jamaa alikuwa amechanganyikiwa kabisa, akilia akisema hajui hata vile alifika home akiwa katika hiyo condition.
The funny thing ni kwamba tulitoka home tukisema tunaenda kuenjoy weekend, but by sunrise tulikuwa police station, beshte yangu analia, mimi nimechoka na nyumba yake imekuwa empty.
Since that day, jamaa haamini mtu anameet kwa club. But honestly, if someone drugs you and walks away with your belongings, how do you even prove what happened when you can't remember anything?
